Seneta wa Mombasa Hassan Omar amepongeza uamuzi wa kuondolewa mashtaka Naibu Raisi William Ruto na mwanahabari Joshua Arap Sang.
Omar alisema kuwa uamuzi huo utapunguza joto la kisiasa lililokuwa likishuhudiwa katika taifa hili, kufuatia kuendelea kwa kesi hiyo kwa muda mrefu.
Akiongea katika hoteli moja jijini Mombasa Siku ya Jumatano, Omar aliwataka viongozi wa pande zote kuangazia zaidi masuala ya ujenzi wa taifa badala ya kupiga siasa duni.
“Serikali kwa ushirikiano na upinzani inafaa kuzingatia kupiga vita suala la ufisadi, pamoja na kuangazia swala la kukuza uchumi na uboreshaji wa miundo msingi ikizingatiwa hakuna tena joto la ICC,” alisema Omar.
Aliongeza kuwa suala la ICC lilichangia kuenea kwa hisia za kikabila katika nchi, pamoja na safari za kila mara za wabunge na viongozi tofauti kuelekea nchini Uholanzi wakati wa kuendelea kwa vikao hivyo.