Gavana wa Mombasa Hassan Joho na aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan omar walipohudhuria kikao cha mahakama. [Photo/Peter Mwangangi]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar ametoa ushahidi wake katika kesi ya kupinga ushindi wa Gavana wa Mombasa Hassan Joho katika mahakama kuu ya Mombasa.Omar alisema kuwa kulikuwa na udanganyifu mwingi wa kura katika vituo mbali mbali Kaunti ya Mombasa.Akitoa ushahidi wake siku ya Jumatatu mbele ya Jaji Lydia Achode, Omar alisema kuwa kuna wapiga kura waliokuwa wanapewa zaidi ya makaratasi mawili ya kupigia kura katika eneo bunge la Changamwe.“Kuna wapiga kura waliopewa zaidi ya makaratasi mawili ya kupigia kura katika eneo la Changamwe. Huu ni wizi wa kura,” alisema Omar.Aidha, Omar alisema kuwa wapiga kura wengi walifurushwa baada ya majina yao kukosekana kwenye vifaa vya Kiems.“Wapiga kura walifurushwa katika vituo vya kura baada ya majina yao kukosekana kwenye kifaa cha Kiems, hatua ambayo ni ukiukaji wa haki za wapiga kura,” alisema Omar.Omar ameitaka mahakama kutupilia mbali ushindi wa Joho na uchaguzi huo kufanyika upya.Kesi ya kupinga ushindi wa Joho iliwasilishwa mahakamani na Omar baada ya Joho kupata ushindi wa kura 221,177 huku Omar akijizolea kura 43,287.