Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Kisii imeanzisha mradi wa kuchimba kisima katika shule ya wavulana ya Amasago kama njia moja ya kumaliza ukosefu wa maji katika shule hiyo. 

Akiongea siku ya Jumatatu katika ofisi yake, mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wavulana ya Amasago, Alloys Mogunde, alipongeza serikali ya kaunti ya Kisii kwa kusikia kilio chao cha ukosefu wa maji katika shule hiyo na kuwasaidia.

Mwalimu mkuu huyo alisema kuwa shida hiyo ikiisha hata wanafunzi watakuwa na muda wa kusoma kwani wakati hawana maji huenda kutafuta maji hayo mbali jambo ambalo wengi wao huwa wanafikiria hata wakati wako darasani.  

“Nimatumaini yangu kuwa tukipata maji hayo hata viwango vya masomo vitaongezeka kwani wanafunzi watakuwa wanatumia muda wao waliokuwa wanatumia kuenda mtoni kusoma," alisema Mogunde. 

Serikali ya kaunti kupitia Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae iliwahakikishia kuwa itachimba Kisima katika shule hiyo ambacho kitasaidia shule hiyo pamoja na Hosplitali ya Keumbu kwani watu wanasumbulka na maji katika eneo hilo. 

Aidha, serikali hiyo ilitoa mtungi wa lita elfu 10 ambao utatumika kuweka maji huku kisima hicho kikiendelea kuchimbwa katika shule hiyo.