Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amefanyia baraza lake la mawaziri mabadiliko.
Katika mabadiliko hayo aliyekuwa waziri wa elimu katika kaunti hiyo John Omwoyo alihamishwa hadi katika wizara ya barababara na uchukuzi huku aliyekuwa waziri wa Maji Skita Ocharo akihamishwa hadi wizara ya Elimu.
Akizungumza siku ya Jumatatu katika afisini mwake Gavana Ongwae alisema kuwa alifanya mabadiliko hayo ili kuleta na kuinua maendeleo zaidi katika kaunti ya kisii.
“Nimefanyia baraza langu la mawaziri mabadiliko ili kuinua maendeleo kwa wakaazi wa kaunti ya Kisii,” alisema Ongwae.
Aidha, Ongwae aliahidi kufanya maendeleo mengi kabla ya mwaka wa ujao, wakati uchaguzi mwingine utaandaliwa nchini.
“Tangu serikali yangu ya kaunti iingie mamlakani tumefanya mengi lakini sijaridhika na nitahikikisha wakaazi wa kaunti hii wamenufaka zaidi kimaendeleo," alisema Ongwae.
"Sisi viongozi tulichaguliwa kufanya maendeleo na kuhakikisha ahadi tulizotoa simetimizwa kikamilifu,” aliongezea Ongwae.