Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema kuwa wako tayari kupokea vifaa vya hospitali kutoka serikali kuu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea katika ofisi yake, Ongwae alisema kuwa wako tayari kupokea vifaa hivyo ili viweze kusaidia sekta ya Afya .

Gavana Ongwae aliongezea kusema kuwa wao kama serikali ya kaunti hawakukataa kupokezwa vifaa hivo, ila walikuwa wanahitaji kuelezwa jinsi ya kupokezwa vifaa hivyo.

“Tuko tayari kupokea vifaa ambavyo vitainuaa viwango vya sekta ya afya, lakini sio kuwekewa masharti ndiposa uweze kupokezwa,” alihoji Ongwae.

Aidha, alisema kuwa serikali yake imeweka sekta ya afya kuwa ya kwanza kushughulikiwa ili kusaidia kila mwananchi wa kaunti, huku akisema kuwa hospitali ya Kisii inasaidia watu wengi kutoka kaunti jirani kama Nyamira, Migori, miongoni mwa nyingine kupata matibabu.

Kwingineko mwakilishi wa wadi ya Kisii ya Kati ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kushugulika sekta ya afya katika mbunge la kaunti ya Kisii Alfred Monyenye amesema kuwa serikali ya kaunti ya Kisii imeweka mikakati kabambe ya kuinuia viwango vya sekta ya afya katika kaunti hiyo.

“Sisi kama kamati inayoshughulikia maswala ya afya katika bunge letu la kaunti, tanaendelea kushirikiana na gavana ili kuweka mikakati kabambe itakayosaidia  mradi huo,” alihoji Monyenye.