Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae amewaomba wasimamizi wote wa shule kushirikiana na serikali yake kupigana na visa vya mikasa ya moto katika kaunti yake .
Mikasa ya moto imekuwa ikiathiri shule mbalimbali na kuchoma bidhaa vya wanafunzi, na kiini cha moto hakijawahi julikana na kuwaomba wasimamizi wa shule kuja pamoja na kutafuta suluhu ya kuchunguza chanzo ya mikasa hiyo.
Alikuwa akiongea mnamo siku ya Jumatatu katika shule ya upili ya St Peters Nyamesocho iliyoko eneo bunge la Bomachoge Borabu kaunti ya Kisii ambapo bweni la wanafunzi 185 lilichomeka siku ya Jumatatu.
Wakati huo huo, gavana huyo alisema ingawa serikali kuu ndiyo inastahili kusaidia ujenzi wa shule, wao kama serikali ya kaunti huwa wanatoa usaidizi maana serikali ya kaunti haiwezi kusubiri mpaka hatua ichukuliwe na serikali ya kitaifa.
“Sisi kama serikali ya kaunti tukiitwa kwa hafla ya kuchangisha fedha ambazo husaidia ujenzi wa shule mbalimbali huwa tunaenda kama serikali ya kaunti na tunasaidia ili wanafunzi wetu waweze kupata elimu ya kiwango kinachostahili,”alisema Ongwae.
Aidha, Ongwae aliahidi kuikabidhi shule hiyo pesa taslimu shillingi 100,000 kutoka mfuko wake ili ujenzi wa bweni ya shule hiyo huweze kukamilika haraka iwezekanavyo, ili wanafunzi warejee kwa masomo yao ya kawaida bila taswishi yoyote.
Ongwae walifika katika shule hiyo ya st Peters wakiwa na Naibu wake Joash Maangi pamoja na Maafisa wake wa usalama.
Shilingi 200,000 zilichangishwa kwa hafla hiyo, huku zikisubiriwa zile gavana ongwae aliahidi kutoa kutoka kwa mfuko wake kuwasilishwa kwa shule hiyo baadaye.