Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema ikiwa viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza sukari nguru vitafungwa katika kaunti ya Kisii basi vifungwe kote nchini ili kuonyesha uwazi

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya kamishina wa kaunti ya Kisii Chege Mwangi kuagiza viwanda hivyo katika eneo bunge la Mugirango Kusini vifungwe kwa kile alichoseme kuwa sukari nguru hutumika kupika pombe haramu.

Kulingana na Ongwae ni haki kwa wakaazi kutengeneza sukari nguru ili kutumika kwa kutengeneza vitu tofauti wala sio kupika pombe haramu.

“Sukari nguru inatengenezwa eneo la Kisii, Magharibi mwa Kenya na sehemu zingine za taifa la Kenya na hakuna vile sukari nguru itaacha kutengenezwa katika eneo la Kisii,” alisema Ongwae.

Wakati huo huo, Ongwae aliahidi kumwandikia barua Kamishina Mwangi ili wajadiliane ili kuondoa agizo hilo kwani wakulima wengi hutegemea miwa kutengeza sukari nguru.

”Wakaazi wa Mugirango Kusini hutegemea sukari nguru na hakuna vile uzalishaji wake utasimamishwa,” aliongeza Ongwae.