Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae, amewaomba watu kutochukua sheria mikononi mwao jambo mbaya linapotokea.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea mnamo siku ya Ijumaa katika mji wa Kisii  wakati wanabodaboda na wanafunzi wa chuo cha Gusii Institute of Technology walizua rabsha katika mji wa Kisii kulalamikia wanafunzi wao waliopoteza maisha yao jana baada ya kuangukiwa na gari lililobeba miti ya stima.

Wakati uo huo, Ongwae  alisema kufanya rabsha, kuandamana na kufunga barabara si suluhisho jambo mbaya linapotokea ila wanapaswa kukaa na kutafuta suluhisho halisi.

“Nawaomba watu wangu msichukue sheria mikononi mwenu ila ni mtafute mbinu mbadala ya kutafuta suluhisho,” alisema Ongwae.

Utulivu umerejea baada ya maafisa wa polisi kuwatawanya watu hao kwa kufyatua marisasi angani na watu hao kuogopa huku wengi wakitoroka .

Funjo hizo ziliwafanya maafisa wa polisi wa vitengo mbalimbali kufika katika mji wa Kisii kuwatawanya waliokuwa wakifanya fujo katika mji wa kisii.

Watu wengi walijeruhiwa wakati maafisa wa polisi walikuwa wakifyatua marisasi angani.

"Ni vibaya sana maafisa wapolisi wakianza kufyatua risasi kiholela jambo ambalo linawasababishia wengine kujeruhiwa," alihoji Moorine Mokeira mkaazi wa Kisii.

Utilivu umerejea katika mji wa kisii ingawa watu wengi walihofia usalama wao baada ya wengi kutorokea uwanja wa mahakama ya Kisii wakiogopa kutotoka nje kwa kusikia milio ya risasi .