Akina mama katika kaunti ya Kisii wameshauriwa kufika katika hospitali kila wakati kupimwa ugonjwa wa saratani ili kujua kama wameathirika na ugonjwa huo.
Akizungumza siku ya Jumatatu mjini Kisii, mke wa gavana wa kaunti ya Kisii Elizabeth Ongwae alisema ni muhimu kwa akina mama kufika katika mahospitali na kupimwa ili kuanza kupata tiba ya mapema kabla ya ugonjwa huo kusambaa mwilini.
Kulingana na Ongwae, akina mama wanafaa kupimwa aina zote za saratani kwani ugonjwa huo umebainika kuwa miongoni mwa magonjwa makali katika mauaji dunini.
“Kila mwanamke anafaa kupimwa ugonjwa wa saratani, na ninawaomba wote kufika katika mahospitali ili kupimwa,” alisema Ongwae.
Wakati huo huo, Ongwae alisema kampeini itaanza ya kutembelea kaunti zote 47 kote nchini ili kukusanya fedha, takribani millioni 50 ambazo zitatumika kupambana na ugonjwa huo nchini.