Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amehimiza serikali ya kitaifa kuongeza mgao wa pesa kwa serikali za kaunti ili kutumika kuimarisha zaidi sekta ya afya ikilinganishwa na jinsi ilivyo kwa sasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na Ongwae serikali ya kaunti ya Kisii hutumia asilimia 46 katika bajeti yake kwa sekta ya afya na kusema ata hivyo haitoshi na kuomba nyongeza ya fedha ili kuimarisha sekta hiyo.

Akizungumza mnamo siku ya Alhamisi katika uwanja wa michezo wa Gusii Ongwae alisema sekta ya afya inafaa kuzingatiwa zaidi huku akiomba pesa kuongezwa kwa kaunti ili kutumika huhakikisha sekta ya afya imeinuka.

“Naomba serikali ya kitaifa kuthamini jinsi sekta ya afya huchukua pesa nyingi naomba mgao wa pesa kwa kaunti kuongezwa ili kuwa rahisi kuimarisha sekta hiyo,” alisema Ongwae.

Aidha, Ongwae aliomba wahuguzi katika kaunti mbalimbali nchini kutogoma kulalamikia matakwa yao na kuwashauri kuwa na mazungumzo na serikali za kaunti ili kuendelea kusaidia wagonjwa kila wakati ili kupunguza hatari kwa wagonjwa.