Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyonka ametangaza msimamo wake kuwa ataiunga mkono serikali ya Uhuru Kenyatta kwa maswala ya maendeleo katika eneo bunge lake.

Akiongea siku ya Jumanne katika shughuli ya kuzindua mradi wa kusafisha mji wa Kisii katika soko la Daraja Mbili lililoko viungani mwa mji huo, mbunge Onyonka, alisema kuwa serikali ya Jubilee imefanya maendeleo makubwa na hayahitaji kupuuzwa na wanasiasa wa upinzani.

Mbunge Onyonka aliwataka wale wanaopinga serikali kwa maswala ya maendeleo kukoma kabisa na kuunga mkono masuala ya maendeleo yanayofanywa na serikali ili kuimarisha uchumi na kuwezesha vijana kuapata kazi za serikali.

"Nipo tayari kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kwa mambo ya maendeleo na nawaomba wale walioko katika chama changu Cord kuyaunga maendelewa yanayobuniwa na serikali ili tisukume mbele kaunti zetu kimaendeleo maanake maendeleo hayajui mipaka ya serikali au upinzani,” aliongeza Onyonka.

Mbunge huyo pia aliwataka wale wanaoeneza uvumi kuwa amehamia mrengo wa serikali ya JAP waache uvumi huo na kufunua kuwa yeye hajahama ila anafanya kazi na serikali kuhusu masuala ya maendeleo tu na si kuwa amehama chama cha Cord na kusistiza kuwa Chama hicho kitakosoa makosa yanapotokea kwenye upande wa serikali.