Mwenyekiti wa chama cha wafanyibiashara wanaoingizaji magari humu nchini yaani ‘Car Importers Association of Kenya’ Peter Otieno, amepinga vikali madai aliyotolewa na mshirikishi mkuu wa utawala eneo la Pwani Nelson Marwa kuwa wafanyibiashara hao wanaingia dawa za kulevya nchini kwa kuzificha kwenye magurudumu ya magari.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye makao na wanahabari katika afisi za chama hicho mjini Mombasa siku ya Jumatano, Otieno amemtaka afisa huyo tawala kudhibitisha madai aliyoyatoa kwani hatua hiyo huenda ikachangia kusambaratisha shughuli za kibiashara za kuingiza magari humu nchini kupitia bandari ya Mombasa.

Otieno amesema kuwa kamwe wafanyibishara hao wajawahi kuingiza dawa za kulevya humu nchini na akamtaka Marwa kuwatia nguvuni wanatekeleza shughuli hiyo wala sio kuingiza dosari katika biashara hiyo.

"Tunamtaka Marwa kuthibitisha madai aliyotowa kuwa sisi tunaingiza mihadarati kwa kuzificha kwenye magurudumu ya magari tunayoleta Mombasa, hiyo sisi tunasema anatuharibia sifa ili kusambaratisha biashara ya magari," alisema Otieno.

Otieno ameahidi kushirikiana na maafisa wa polisi kuwatia nguvuni watu kama hao iwapo wanatekeleza shughuli hiyo kwani wanaharibu sifa za wafanyibiashara hao huku akizidi kusema kuwa kamwe wafanyibishara hao hawahusiki na shughuli za dawa za kulevya.

Awali mshirikishi mkuu wa utawala eneo la Pwani Nelson Marwa alitangaza kuchunguzwa kwa wafanyibishara wa wanaoingiza magari nchini kupitia bandari ya kutokana na madai kuwa wanaingiza dawa za kulevya kwa kuzificha kwenye magurudumu ya magari, madai ambayo yamezua hisia mseto.