Mwanasiasa kutoka eneo bunge la Nyaribari Chache Zaheer Jhanda ambaye pia aliwania kiti cha ubunge mwaka wa 2013 amesema pesa za hazina ya ustawi maeneo bunge, CDF, hazitumiki vizuri katika bunge hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza siku ya Jumapili katika eneo la Kiogoro, eneo lililoko katika bunge hilo, Jhanda alisema eneo hilo limerudi nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na maeneo bunge mengine kufuatia kutotumiwa kwa pesa za CDF vizuri.

“Wakati viongonzi waliochaguliwa hawazitumii pesa inavyostahili, haswa kwa maendeleo, sisi vijana lazima tuwambie na warekebishe. Sisi tunahitaji kuona maendeleo yakifanywa kikamilifu kwa wanachi wote kwa usawa,” alisema Jhanda.

Wakati huo huo, mwanasiasa huyo aliungwa mkono na vijana wengine, huku wakisema kuwa waliwachagua viongonzi kufanya maendeleo.

“Viongonzi wote waliochaguliwa wawe wawakilishi, na mbunge wa eneo hili mheshimiwa Richard Tong’i tunawahitaji hao wote kuturidhisha kimaendeleo ili eneo letu liweze kuinuka kimaendeleo,” alihoji Zablon Nyakundi, mkaazi wa eneo hilo.

Vijana hao wameomba pesa za CDF kutumiwa vizuri katika eneo hilo kama njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafaidika kimaendeleo.

“Wakifanya maendeleo vile tunataka, hatuna lolote la kuwakosoa, lakini sasa ukiangalia hakuna maendeleo na hiyo inatulazimu kuwaamsha kuyafanya maendeleo hayo, la sivyo wakati mwingimne wananchi wanajua la kufanya dhidi ya viongonzi walio kwa viti katika uchaguzi ujao,” aliongezea Jhanda.