Share news tips with us here at Hivisasa

Bodi ya uchaguzi wa kitaifa katika chama cha ODM imetatua mzozo ambao umekuwepo kwa miezi mitano sasa kati ya makundi mawili ya chama hicho tawi la Nakuru.

Makundi hayo yalikuwa yameandaa uchaguzi mwaka jana ulioshuhudia kuchaguliwa kwa viongozi katika kila kundi,  huku kila kundi likishikilia kwamba ndilo halali, tofauti ambazo zilisambaratisha shuguli za chama hicho mjini humu.

Jumapili, bodi hiyo chini ya mwenyekiti Judith Pareno, katibu Nyaigoti Chacha na mkurugenzi mkuu Oduor Ongwen,   ilimwidhinisha mwanasiasa mkongwe kutoka Gilgil mjini Peter ole Osono kama mwenyekiti halali wa chama hicho katika jimbo la Nakuru.

Lumumba Chanzu aliteuliwa katibu ili hali Hezron Odhiambo atakuwa katibu mwandalizi.

Orodha hiyo ya wanasiasa wanaoegemea upande wa ole Osono ilitolewa jumatatu katika ofisi ya chama hicho mjini Nakuru, huku muungano mwingine unaoongozwa na Moses Abiola ukisusia mkutano huo kwa madai ya mapendeleo.

“Tumesuluhisha mzozo uliokuwa kati ya makundi mawili hapa Nakuru na kusababisha shuguli kukwama,” alisema mwenyekiti Pareno