[Picha/courtesy]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Jamii ya wakamba mjini Mombasa imeapa kwa kauli moja kumuunga Mkono Peterson Mitau kama mgombeji wa kiti cha ubunge cha Changamwe.Jamii hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa baraza la wazee Samy Kisilu imetoa kauli hiyo kutokana na kile wanachodai ni dhulma wanazodai alitendewa kiongozi huyo wakati wa kura ya mchujo wa chama cha wiper hapa mombasa.Wanadai kuwa Daniel Muange aliyepewa tiketi ya kuwania ubunge wa eneo hilo na chama cha Wiper hajaonyesha hari ya kuongoza wakaazi wa changamwe na hivyo basi kauli yao ni kumuunga mkono Mitau.Mitau ametangaza kuwa atatoa uongozi Mbadala kwa wenyeji wa eneo hilo huku akimsuta mbunge wa eneo hilo Omar Mwinyi kwa uwongozi mbaya.