Mshukiwa mmoja wa unajisi anazuiliwa katika kituo cha polisi cha bondeni baada ya kudaiwa kuwanajisi watoto wanne katika mtaa wa Abong’oloya viungani mwa mji wa Nakuru.
Mshukiwa huyo kwa jina Harun Chitwa , anandaiwa kutekeleza unyama huo kwa watoto hao wasichana wa kati ya umri wa miaka minne na nane siku ya Jumatatu.
Mama mmoja ambaye mtoto wake msichana anadaiwa kubakwa alidai kuwa mshukiwa huyo ambaye anajulikana sana kwa kuvuta bangi na kunywa pombe, amekuwa akimhangaisha mamake mzazi.
Watato hao waliwaeleza wazazi wao kilichofanyika na ndipo hatua zikachukuliwa na mshukiwa kukamatwa.
Kwa sasa watoto hao wanapelekwa kwa uchunguzi wa kimatibabu katika hospitali kuu ya kaunti.
Polisi hawakutoa ripoti zozote kuhusiana na kisa hicho.