Maafisa wa polisi katika eneo la Kisauni wameaanzisha uchuguzi dhidi ya madereva wa tuktuk na pikipiki wanaodaiwa kuhusika katika visa vya uhalifu.
Mkuu wa polisi katika eneo la Kisauni Richard Ngatia, amesema kuwa maafisa wa usalama watafanya uchunguzi kwenye vituo vya kuegesha pikipiki na tuktuk, kama njia moja wapo ya kutatua tatizo la visa vya mara kwa mara vya utepetevu wa usalama katika eneo hilo.
“Matamshi ya wahudumu hao kupinga kuhusika katika visa vya uhalifu vitadhihirika baada ya maafisa wa usalama kukamilisha uchunguzi wao. Maafisa wangu watazikagua pikipiki na tuktuk hzote katika eneo hili haswa zinazo hudumu nyakati za usiku,” alisema Ngatia.
Aidha, OCPD huyo alisema kuwa ikiwa maovu yanayotekelezwa eneo la Kisauni yanatarajiwa kupungua, basi ni sharti wakaazi na wafanyabiashara wa eneo hilo kuwaruhusu polisi kuendesha uchunguzi wao bilavikwazo ili wanaowasadia vijana kutekeleza maovu waweze kukamatwa.