Idara ya polisi katika eneo bunge la Kisauni imefanikiwa kupata bunduki kwenye gari linalodaiwa kutumumiwa na majambazi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akithibitisha kupatikana kwa silaha hiyo, Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Kisauni Richard Ngatia, alisema kuwa walifanikiwa kupata bunduki mmoja pamoja na stakabadhi bandia za polisi kwenye gari lililokuwa likitumiwa na washukiwa wa ujambazi.

Haya yanajiri baada ya washukiwa wanne wa wizi kunusurika kifo baada ya jaribio lao la kulivamia gari la kampuni moja ya kusafirisha pesa kutibuka katika eneo la Bamburi, Kisauni.

Akizungumza siku ya Jumatatu, Ngatia alisema kuwa genge hilo lilifanikiwa kutoroka huku mshukiwa mmoja akipigwa risasi.

"Genge hilo lilikabiliana na maafisa wa polisi kabla ya kufanikiwa kutoroka. Mshukiwa aliyepigwa risasi alifikishwa katika Hosipitali kuu ya Makadara,” alisema Ngatia.