Maafisa wa polisi wa kituo cha Kisii wamewatia mbaroni washukiwa watatu wa ujambazi waliomvamia afisa mmoja wa kitengo cha ujasusi usiku wa siku ya Jumatatu katika soko la Nyakoe eneo bunge la Kitutu Chache.

Share news tips with us here at Hivisasa

Inaarifiwa washukiwa hao ambao ni wavulana walimvamia afisa huyo alipokuwa anapita katika soko hilo akielekea kwake.

Akizungumza siku ya Jumatano mjini Kisii, kamanda wa polisi katika kaunti ya Kisii Agnes Elhaba alisema afisa huyo aliyevamiwa aripiga ripoti kwa kituo ha polisi kisha maafisa wa polisi wakaanzisha uchunguzi wao.

“Washukiwa hawa walimvahamia afisa wa kitengo cha ujasusi alipokuwa anaelekea nyumbani kule Nyakoe sasa alipofika kwa soko la eneo hilo ndiposa alikutana na vijana ambao walijifanya kuwa waendeshaji pikipiki kisha kumnyanganya simu na pesa, kwa sasa wako kwa jela wakisubiri kushtakiwa ,” alisema Agnes Elhaba.