Jengo la Mahakama ya Mombasa.[Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Afisa mmoja wa polisi amefunguliwa mashtaka ya mauaji katika mahakama kuu ya Mombasa.Stephen Omondi kutoka kituo cha polisi cha Changamwe, anadaiwa kumuua Jackson Mwangi kwa kumpiga risasi mnamo Octoba17, 2017, katika eneo la Changamwe.Omondi hata hivyo alikanusha mashtaka hayo siku ya Jumatano mbele ya Hakimu Dora Chepkwonyi."Sikuhusika katika mauaji ya mwendazake. Hizo ni njama za kunikandamiza,” Omondi aliambia mahakama.Jaji Chepkwonyi aliagiza Omondi kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 500,000. Akitoa uamuzi huo, Hakimu Chepkwonyi alisema kuwa ni haki ya kila mshukiwa kupewa dhamana kwa mujibu wa katiba.“Dhamana ni haki ya kila mshukiwa anayekabiliwa na mashtaka yoyote kwa mijibu wa katiba,” alisema Chepkwonyi. Kesi hiyo itasikizwa tarehe Machi 8, 2018.