Maafisa wa usalama eneo la Likoni wanamzuia mwanamume wa miaka 43 kwa madai ya ulawiti.
Mshukiwa huyo, Peter Malakisi, anadaiwa kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka saba katika eneo la Mtongwe, Likoni.
Malakisi anadaiwa kumnajisi mtoto huyo, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi ya kibinafsi ya South Gate juma lililopita.
Mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba alisema inadaiwa kwamba Malakisi alimuita mtoto huyo na kumdanganya kwamba atamnunulia peremende.
“Tumepata taarifa kwamba alimdanganya mtoto huyo kwa peremende, kisha kutekeleza kitendo hicho,” alisema Simba.
Malakisi ni mlinzi wa shule hiyo ya South gate.