Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kamishena wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amewakashifu maafisa wa polisi na machifu ambao wanachukua hongo kutoka kwa wagema.

Kamishena huyo alisema kuwa hiyo ni kinyume na sheria na kutoa amri kuwa yeyote atakayepatikana akipokea hongo hiyo atafutwa kazi na kuchukuliwa hatua kali na serikali.

Akizungumza siku ya Jumanne katika mkutano alioandaa na machifu wote wa kaunti nzima ya Nyamira pamoja na maafisa wakuu wa polisi, kamishena huyo alisema kuna ripoti ambazo amepokea kuwa kuna baadhi ya maafisa wa polisi pamoja na machifu ambao wanaruhusu biashara hiyo kuendelea kwa kupokea hongo kutoka kwa wagema.

“Afisa yeyote na chifu yeyote atakayepatikana akichukua hongo atasimamishwa kazi na kuenda nyumbani. Vita dhidi ya pombe haramu vitaendeleo na maafisa wa polisi wanapswa kukoma kutimia njia hiyo kupata pesa,” alisema Onunga.

Wakati huo huo, kamishena Onunga alipongeza wale wameshirikiana naye kupambana na uuzaji wa pombe haramu kwa kumwagwa pombe hiyo katika sehemu mbalimbali za kaunti hiyo ya Nyamira.

Alisema kuwa washukiwa wale wanatiwa mbaroni wafikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya kufanya biashara hiyo ambayo ilikanwa sarikali.

“Kufikia sasa tumemwaga chang’aa lita 1000 na lita 8,000 za kangara katika kaunti ya Nyammira na tunaendelea na umwagaji huo wa pombe haramu,” alisema kamishena Onunga.