Naibu mkuu wa polisi gatuzi dogo la Kisauni Walter Abondo akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Picha/ nation.co.ke]
Idara ya polisi Mombasa imekanusha madai kuwa ilimpiga risasi kimakosa kijana mwenye umri wa miaka 17 katika mtaa wa Kambi Kikuyu.
Haya yanajiri baada ya kijana huyo, Arafa Ramadhan, kupigwa risasi siku tatu zilizopita.Naibu mkuu wa polisi gatuzi dogo la Kisauni Walter Abondo amesema kuwa kijana huyo ni miongoni mwa washukiwa wa ujambazi ambao wamekuwa wakisakwa na maafisa wa polisi.“Kijana huyo ni mmoja wa majambazi sugu ambao wamekua wanasakwa na polisi kwa muda mrefu na alikuwa akikwepa mitego ya polisi kila mara,” alisema Abondo.Abondo alisema kuwa wanasubiri kijana huyo kupata nafuu ili aweze kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka.Aidha, Abondo alisema kuwa polisi watawanasa majambazi wanaotatiza amani katika eneo hilo.Kauli yake inajiri baada ya familia ya kijana huyo kudai kuwa kijana huyo alipigwa risasi mwendo wa saa saba usiku alipokua akidai simu yake iliyokua imeibiwa.