Mbunge wa Nyali Hezron Awiti ameitaka serikali hasa idara ya polisi kukoma kuwahangaisha wanawake ambao hufanya biashara ya kuuza pombe ya mnazi.
Mbunge huyo alisema kuwa maafisa wa polisi wanawadhulumu watu wanaofanya biashara hiyo.
Aidha, Awiti alisema kuwa pombe ya mnazi si haramu na kwa hivyo wanaofanya biashara hiyo wanafaa kuendesha biashara yao bila ya kuhofia usalama wao.
Kauli ya Awiti iliungwa mkono na Mshirikishi wa Usalama katika ukanda ya Pwani Nelson Marwa ambaye amewataka wanawake hao kufanya biashara hiyo kwa kuzingatia muda uliowekwa na serikali.
“Pombe ya mnazi iliwekwa huru kwa matumizi ya binadamu lakini sheria lazima ifuatwe,” alisema Marwa.
Pombe ya mnazi hupatikana sana katika maeneo ya Pwani.