Maafisa wa polisi katika eneo la Kisauni waendelea kusaka wanachama wa genge la wahalifu linalowangaisha wakaazi na kuwapora mali yao.
Akizungumza siku ya Jumatano, afisa mkuu wa polisi eneo la Kisauni Richard Ngatia, alisema kuwa polisi walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili waliokuwa wakipora mali ya wakaazi katika maeneo ya Mgongeni, Katishia na Frere town.
Ngatia alisema kuwa majambazi hao waliouawa siku ya Jumanne walikuwa wanachma wa genge la vijana la Wakali Kwanza linalohangaisha wakaazi katika eneo hilo.
Ngatia ameahidi kukabiliana na genge hilo kikamilifu ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.
"Tumejitolea kikamilifu kuimarisha usalama na lazima magenge ya kihalifu Kisauni kukabiliwa,” alisema Ngatia.