Maandamano ya kupinga tume ya uchaguzi na mipaka mjini Mombasa yametawanywa na polisi ambao walikuwa wameuzingira uwanja wa Uhuru Gardens ili kuwazuia kukusanyika humo ndani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Maandamano hayo yaliyotarajiwa kuanza saa tatu unusu na kuongozwa na gavana Hassan Joho ambaye pia ni naibu kiongozi wa ODM yalipata pigo wakati polisi waliwarushia vitoa machozi.

Polisi wamemtia mbaroni spika wa bunge la kaunti ya Mombasa Thadius Rajwayi na mwakilishi wadi wa Junda Paul Onje.

Wawili hao wamepelekwa katika kituo cha Mombasa.

Maduka ya biashara yalibakia kufungwa huku polisi wakikabiliana na waandamanaji waliokuwa wakibeba mabango na vitambaa vyeupe.