Polisi mjini Naivasha wamemtia nguvuni mshukiwa mmoja anayeaminika kuwa sugu kuhusiana na kifo cha dereva mmoja wa trela aliyeuawa wiki mbili zilizopita.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa huyo mwenye umri wa makamo ametiwa nguvuni mapema Alhamisi na anaendelea kuzuiliwa hadi pale uchunguzi utakapokamilika.

Kwa mujibu wa polisi, mshukiwa huyo mwenye umri wa makamo alikuwa katika genge la majambazi waliokuwa wakijaribu kuteka nyara trela hilo kwenye barabara kuu ya kuelekea Mai Mahiu kutoka Naivasha.

Aidha washukiwa hao walikuwa wameamrisha dereva huyo kuliendesha trela hilo na alipokaidi amri hiyo walimuua kwa kumnyonga.

Afisaa mmoja wa polisi ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema kuwa: "Tunamhoji mshukiwa huyo ili kujaribu kuwanasa wenzake kabla ya kumfikisha mahakamani."