Kamanda wa polisi kwenye kaunti ya Nakuru Hassan Barua amewaonya vikali wale walio na lengo la kuvuruga amani na kufanya vitendo vya kigaidi kwenye kaunti ya Nakuru.
Akizungumza Jumanne, Barua alionya kuwa yeyote atakayepatikana na hatia hii atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Barua aliwataka wakaazi wa Nakuru kufikisha ripoti kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu nao.
Wakati huo huo, aliwahakikishia wakaazi wa Nakuru usalama wao akisisitiza kuwa usalama umeimarishwa kote kwenye kaunti ya Nakuru.
Katika harakati za kuimarisha usalama, aliweka bayana kuwa doria za polisi zimeimarishwa na kuwa vikosi vya kushika doria vimetumwa katika sehemu mbalimbali za kaunti kuhakikisha kuwa usalama wa umma umeimarishwa.