Afisa wa polisi tawala anayesimamia operesheni ya kukabiliana na pombe haramu katika kaunti ndogo ya Nakuru Mashariki Barnabas Kimutai amesema hatakoma kukabiliana na pombe haramu katika eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na mwandishi huyu Alhamisi baada ya kumnasa mmoja wa wale wanaouza pombe hiyo haramu katika mtaa wa Kanyon viungani mwa mji wa Nakuru, Kimutai alisema kuwa, wameanzisha msako usiku na mchana wa maeneo yanayoshukiwa kuendesha biashara hiyo haramu.

"Mtu mmoja kwa jina la Daniel Theuri Wangare ambaye ni , mkaazi wa Kanyon ni mpishi sugu wa pombe haramu . Amekuwa akikwepa mtego wetu kwa muda mrefu. Siku yake ya arobaini ilifika. Tulimpata na lita 47 za Chang’aa, lita 1,000 ya Kang’ara na vifaa anavyotumia kutengeza pombe yake," alisem Kimutai.

Huku akishukuru umma sawa na viongozi wa nyumba kumi katika eneo hilo, Kimutai amewatolea wito wananchi kuendelea kushirikina na polisi ili kumnaliza pombe hiyo.

"Upishi na uuzaji wa Pombe haramu umepungua. Hii ni kutokana na juhudi za wanachi pamoja na uwepo wa mradi wa nyumba kumi. Nahimiza wanachi kuzidi kutupasha habari ili upishi na uuzaji wa Pombe haramu ukabiliwe kabisa Nakuru," aliongeza Kimutai.