Idara ya usalama jijini Mombasa imeanzisha uchunguzi dhidi ya wanasiasa wanaodaiwa kufadhili makundi haramu ya vijana.
Kamisha wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki amesema kuwa uchunguzi unaendelea na watakaopatikana watachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumanne katika afisi yake, Achoki alisema kuwa kuna baadhi ya magenge ya uhalifu yanayofadhiliwa na viongozi wenye malengo ya kutatiza usalama jijini Mombasa huku uchaguzi mkuu unapowadia.
“Nawahimiza vijana kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa katika kutekeleza vurugu na uahalifu. Watakao patikana wakishiriki uhalifu wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Achoki.