Maafisa wa polisi wilayani Manga kaunti ya Nyamira wameanzisha msako wa kumsaka msichana mmoja wa umri wa miaka 17 kutoka kijiji cha Morambe baada ya kuafia mimba ya miezi saba na kutupa ndani ya choo ya jirani yake.
Hii ni baada ya maafisa hao kupokezwa habari kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, jambo lililopelekea msako mkali kuanzishwa ili kupatikana na kushtakiwa kwani ni kinyume na sheria.
Akizungumza siku ya Jumanne katika eneo la Manga, chifu wa lokesheni ya Central Kitutu Evans Nyang’au alisema msichana huyo amekuwa na mimba kwa mda mrefu, huku ikibainika kuwa alitoa mimba hiyo na kuirusha ndani ya choo.
“Tulipata habari kutoka kwa wakazi wa kijiji cha Morambe kuwa msichana huyo ametoa mimba ambayo ilikuwa ya miezi saba na akakimbilia mafichoni, lakini sasa tumeanzisha msako wa kumtafuta,” alisema Nyang’au.
Chifu huyo aliomba wakazi haswa wasichana kutotoa mimba kwani sheria hairuhusu hayo.