Maafisa wa polisi wameanzisha msako wa kuwasaka washukiwa watatu ambao walimchoma ajuza mmoja kwa madai ya kuwa mchawi katika kijiji cha Ng’eri wilayani Kisii Kusini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Washukiwa hao walimchoma ajuza huyo wa miaka 75 kwa jina Maria Matibe siku ya Jumanne mchana kwa madai kuwa mchawi.

Akizungumza katika eneo hilo la Ng’eri mkuu wa polisi wilayani Kisii Kusini Ngonja mwero alisema washukiwa hao watatu ni majirani wa ajuza huyo ambao walimshuku kuwa mchawi na kumchoma huku akisema baada ya kutekeleza kitendo hicho washukiwa hao walitoroka na maafisa wa polisi wameanzisha msako kuwatia mbaroni.

“Ni vibaya sana wakati mtu anachukuwa sheria mikononi mwake na washukiwa hao tutawatafuta hadi tuwatie mbaroni,” alisema Mwero.

Maafisa wa polisi wa kituo cha Riana walifika eneo hilo na kupeleka mwili wa marehemu hadi chumba cha kuhifadhi maiti huku uchunguzi ukiendelea kufanywa.