Idara ya polisi jijini Mombasa inachunguza kisa kimoja ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 30 alifariki baada ya kushuka kutoka kwa feri.
Akidhibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi katika eneo la Likoni Willy Simba, alisema kuwa mwanamume huyo alianguka na kuzirai baada ya kushuka kwa feri mwendo wa saa tano mchana siku ya Jumatatu.
Simba alisema kuwa mwili wa mwanamume huyo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Makadara ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.