Waziri Joseph Nkaissery amesema idara ya usalama imepata mafunzo ya kukabiliana na visa vya uchochezi nchini, wakati huu ambapo taifa linakaribia uchaguzi mkuu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza kwenye kongamano la kujadili jinsi taifa litakavyoandaa uchaguzi huru na wa amani katika hoteli moja huko Diani, Kaunti ya Kwale, Nkaissery alisema mkono wa sheria hautamsaza kiongozi yoyote atakayepatikana akieneza chuki miongoni mwa wananchi katika mikutano ya hadhara.

Aidha, waziri huyo amesema zaidi ya kamati 300 za usalama wa jamii al maarufu kama Nyumba Kumi, zimeanzishwa ili kueneza amani na kupiga vita ugaidi.

Wakati huo huo, Nakaiserry alinyoshea kidole cha lawama idara ya mahakama kwa kuwaachilia wahalifu kwa dhmana bila kuzingatia athari wanazotenda kwa taifa.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Tume ya uwiano na utangamano nchini NCIC, Francis Ole Kaparo amewataka Wakenya kudumisha amani kote nchini.

Kaparo alisema kuwa kuwepo kwa tofauti za kisiasa kutasambaratisha uchumi wa taifa.

Amewataka wanasiasa kuacha matamshi ya chuki wanapokuwa katika mikutano ya hadhara, hatua aliyosema husababisha migawanyiko miongoni mwa wananchi.