Kamanda mkuu wa polisi katika ukanda wa Pwani Francis Wanjohi amesema kuwa maafisa wa polisi walioshuhudia mama akivuliwa nguo wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi mnamo Machi 7, watashtakiwa.
Akizungumza kwenye mahojiano na mwandishi huyu siku ya Jumatatu, kamanda huyo alisema maafisa hao walikiuka maadili ya afisi yao kwa kumtazama mama huyo akivuliwa nguo pasi kuchukua hatua yoyote wala kumsaidia.
Kulingana na Wanjohi maafisa hao tayari wameandikisha taarifa katika makao makuu ya idara ya polisi eneo la Pwani.
Aidha, Wanjohi alisema kwamba gari lililokuwa likitumika na maafisa hao lilikuwa katika eneo ambapo makundi ya uhalifu kama vile Wakali Wao na Wakali Kwanza yanadaiwa kusafirishwa na baadhi ya wanasiasa na wafanyibiashara kwa lengo la kuvuraga zoezi hilo.