Wakaazi wa eneo la Bokeira, wilayani Nyamira kaunti wameomba maafisa wa polisi katika eneo hilo kuimarisha usalama baada ya visa vya utovu wa usalama.
Hii ni baada ya mwanamme mmoja kupiwa risasi kadhaa na kuawa katika kijiji cha Nyakaranga, eneo la Bokeira na majambazi wasiojulikana huku mkewe na watoto wake wawili wakijeruhiwa.
Wakizungumza siku ya Jumapili, wakazi hao walisema wameofya maisha yao, na kuomba maafisa wa polisi kuimarisha usalama katika eneo hilo kwa kupiga patroli haswa nyakati za usiku kuhakikisha wakazi hao hawavamiwi.
“Tumekuwa tukilia na wenzetu wanaendelea kuawa, tunaomba maafisa wa polisi kutusaidia kwa kuimarisha usalama katika eneo hili,” alisema John Mokua, mkazi.
“Tunaomba kamishena wa kaunti yetu Josephine Onunga kuwatuma maafisa wa polisi kuimarisha usalama katika kaunti nzima ya Nyamira ili visa vya uvamisi kupunguzwa,” alisema Lilian Bonareri, mkazi mwingine.