Idara ya polisi katika eneo la Pwani inaonya huenda wanamgambo wa Alshabab wakafanya shambulzi la kigaidi humu nchini hasa maeneo ya Pwani na magharibi mwa nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kamanda wa polisi eneo la Pwani Francis Wanjohi amewatahadharisha Wapwani kuwa waangalifu zaidi na kuripoti kwa maafisa wa polisi washukiwa wa ugaidi ili kukabiliwa vikali.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Wanjohi kuwa tayari maafisa wa usalama wametuma kila sehemu kushika doria na kuzuia kushughudiwa kwa visa vya mashambulizi ili kuona kuwa eneo la Pwani iko salama.

"Tumetuma maafisa wetu kila mahali kushika doria na kulinda wananchi na tunawahimiza wananchi kuwa washirikiane na maafisa wa polisi  na kutoa habari kuhusu washukiwa wa ugaidi ili watiwe nguvuni mara moja," alisema Wanjohi.

Aidha amesema kuwa kutokana na kuimarishwa kwa vita dhidi ya wanamgambo hao nchini Somalia, kuna uwezekano kuwa baadhi yao wanaeza kukimbilia nchini, na kujaribu kutekeleza shambulizi.

Kauli ya Kamanda huyo mkuu wa polisi eneo la Pwani imejiri baada ya taarifa kuhusu njama ya kufanywa mashambulizi humu nchini na Alshabba kutolewa kwa wamiliki wa hoteli, wahudumu wa magari za umma, na Wakenya kwa jumla kuwa waangalifu na kuripoti kisa chochote kisicho cha kawaida.