Mwenyekiti wa IPOA Macharia Njeru katika hafla ya awali. [Picha/ the-star.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Maafisa wa polisi wameshauriwa kutoa ulinzi wa kutosha kwa wananchi hasa katika kipindi hiki cha kampeni na uchaguzi.

Mwenyekiti wa mamlaka ya kutathmini maadili ya maafisa wa polisi nchini IPOA, Macharia Njeru, amezitaka idara mbalimbali za polisi kutotumiwa vibaya na wanasiasa.

“Musikubali kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao ili kukandamiza wananchi,” alisema Njeru.Akizungumza jijini Mombasa, Njeru aliwataka polisi kutotumia nguvu kupita kiasi na badala yake kujizatiti katika shughuli za kuwalinda Wakenya.“Musitumie nguvu na kuwanyanyasa raia bali muwe mstari wa mbele kushirikiana nao,” alisema Njeru.Wakati huo huo, amewashauri wananchi kutokubali kuchochewa kisiasa na kuvunja sheria na badala yake kudumisha uhusiano kati yao na maafisa wa polisi ili kuwe na amani.“Wananchi tafadhali musikubali kuchochewa na wanasiasa kuzua fujo bali tuishi pamoja kwa amani na upendo,” alisema Njeru.