Maafisa wa polisi wamewatia mbaroni mwanamume mmoja na mkewe baada kwa madai ya kumuua jirani yao katika kijiji cha Iyabe eneo bunge la Bonchari kaunti ya Kisii.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume huyo kwa jina Ambrose Kerage na Mkewe walidaiwa kumuua jirani yake siku ya jumapili baada ya kugombana kwa muda mrefu.

Akitibithisha kisa hicho siku ya Jumapili mkuu wa polisi katika eneo hilo Ngoja Ngwero alisema ripoti ambazo alipokea kutoka kwa familia ya wawili hao ambao walitiwa mbaroni ni kuwa walifanya kitendo hicho baada ya kugombana.

“Kulingana na ripoti ambazo tumepewa kutoka kwa familia za waliotiwa mbaroni ni kuwa wawili hao waligombana na walishuku marehemu kuwa mchawi baada ya kudai kuwa alimroga mwenzao ambaye alifariki siku chache zilizopita,” alisema Ngoja Ngwero mkuu wa polisi Bonchari.

Marehemu Simon Mogire alipelekwa hadi chumba cha kuhifadhi maiti cha Nyangena mjini Kisii huku uchunguzi ukiendelea.

Washukiwa hao wawili wa mauaji nao walipelekwa hadi kituo cha polisi cha Gesonso Bonchari.