Kwa mara nyingine tena maandamano ya wanacord katika kaunti ya Nyamira yatibuliwa na wanapolisi hii leo, Jumatatu.
Kulingana mkuu wa polisi kituo cha Nyamira bwana Alex Mumo, waandamanaji hao waliamurishwa kusitisha maandamano hayo, lakini kwani hawakuwa na kibali cha kuandamana.
"Nawaomba mrudi mlikotoka na mrejee shughuli zenu za siku mwachane na maandamano haya kwa kuwa hamna kibali cha kuandamana katika mtaa huu," alisema Mumo.
Wiki jana siku ya Jumatatu afisa huyo vile vile aliyatibua maandamano hayo kwa kuwaomba wayasitishe, na waltii amri ya afisa na kurudi kwelekea makao bila kuzusha fujo hata kidogo.
Wanacord hao walikuwa akiongozwa na kinara wa walio wengi kwenye bunge la kaunti Laban Masire, mweka hazina wa ODM katika kaunti Peter Maroro, na viongozi wengi wa Cord.
vile vile waliahidi kwendelea na maandamano yao hadi makamishena hao wangatuke afisini.