Polisi mjini Mombasa wametumia vitoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Cord waliokuwa wakiandamana kushinikiza Tume huru ya mipaka na uchaguzi IEBC kubanduliwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wafuasi hao walikuwa wamekusanyika katika eneo la Uhuru gardens wakiongozwa na vigogo wa mrengo huo Kaunti ya Mombasa, tayari kuanza maandamano hayo.

Katika kikao na waandishi wa habari siku ya Jumamosi, viongozi hao wakiongozwa na Kalonzo Musyoka waliwataka wafuasi wao kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha maandamano hayo.

Akizungumza siku ya Jumatatu kabla ya maandamano hayo kuanza, Gavana Hassan Joho aliwataka wafuasi wake kudumisha amani wakati wa zoezi hilo.

Joho alisema kuwa ana amini maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ghasia hawatatatiza maandamano hayo kwani hawanuii kutekeleza uharibifu wowote katika maeneo watakayoandamana.

Kwa sasa makabiliano baina ya polisi na wakaazi yanaendelea kushuhudiwa katika eneo la Majengo na sehemu za barabara ya Docks kuelekea Bandari ya Mombasa.