Polisi katika eneo la Likoni wamewatia mbaroni washukiwa wanne wa ujambazi.
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa upelelezi eneo la Likoni Henry Ndombi alisema washukiwa hao walinaswa katika chumba kimoja cha kukodi.
Ndombi alisema wanne hao, wanaume wawili na wanawake wawili, walikamatwa baada ya umma kutoa ripoti kwa kikosi maalum cha polisi.
Aidha, alisema kuwa wawili kati ya washukiwa hao wamo katika orodha ya washukiwa sugu ambao wamekuwa wakisakwa na polisi kwa muda sasa.
Kulingana na Baraka FM, mmoja wa washukiwa hao alikuwa na majeraha ya risasi mwilini, anayodaiwa kupata alipokuwa akitekeleza wizi.