Serikali ya kitaifa kupitia wizara ya usalama wa ndani imeombwa kubadilisha maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Riotonyi kaunti ya Nyamira kwa madai ya kutowajibikia kazi yao.
Akizungumza siku ya Jumatatu katika eneo la Borabu mwanasiasaYobesh Nyandoro Kambi alisema maafisa wa polisi katika kituo hicho wamekaa katika kituo hicho zaidi ya miaka 15 na ni wa kabila moja jambo ambalo limechangia kutowajibikia kazi yao na kudorora kwa usalama.
“Maafisa ambao wako katika kituo cha Riotonyi hawafanyi kazi inavyostahili. Naomba serikali ya kitaifa kubadilisha maafisa hao,” alisema Kambi.