Producer maarufu kutoka Pwani, Khalid, kwa sasa anakabiliwa na hofu ya kukabiliwa na mkono wa sheria baada ya kubainika kuwa alimhusisha kidosho ambaye hajahitimu umri wa miaka 18 katika video yake.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na Khalid, msichana huyo, ambaye anajulikana kama Joy, alikubaliwa kwenye utayarishaji wa video hiyo baada ya kuonekana kwenye video ya msanii mwingine kutoka Nigeria.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio hapa Mombasa, Khalid alisema baada ya kujuana mwezi mmoja uliopita, Joy alimwambia kuwa ana umri wa miaka ishirini na miwili, jambo ambalo lilimfanya Khalid kumruhusu kwenye uandaaji wa video hiyo.

Kwa upande wake, mamake Joy alikiri kuwa mwanawe alizaliwa mwaka wa 1999 na wala hajafikia umri wa miaka 18 kama ilivyodaiwa.

Video ya ngoma hiyo ambayo kwa sasa inaendelea kuzua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha Joy akiwa nusu uchi, jambo ambalo ni kinyume na sheria za uandaaji wa filamu nchini kwa mtoto asiye na umri wa miaka 18.

Tayari mashabiki wamecharuka kiasi cha haja kwenye mitandao huku wengi wakitaka Khalid achukuliwe hatua za kisheria, nao wengine wakisema kuwa msichana mwenyewe anamakosa kwa kukubali kutoka kwenye video hiyo.