Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Nakuru wametakiwa kupunguza joto la kisiasa huku wakijuzwa kwamba bado ni mapema kuanza kampeni zao za kuwania viti mbalimbali vya kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao.

Wito huo umetolewa na viongozi wa Baraza la Rift Valley Council of Elders kupitia kwa taarifa ambayo walitoa Alhamisi.

Katika taarifa hiyo iliyosomwa na mwenyekiti wao Gilbert Kabage, wazee hao walisema kwamba wakaazi wa Nakuru na wananchi kwa jumla wangali wanahitaji maendeleo na wala sio siasa.

Wazee hao walisema kwamba inasikitisha kuona viongozi katika kaunti ya Nakuru wakijihusisha na maswala ya kisiasa bila ya kuzingatia Maendeleo huku Kabage akisisitiza kwamba kutokana na joto la kisiasa ambalo limejitokeza kwa sasa kwenye kaunti ya Nakuru maendeleo yamekwama.