Rais Uhuru Kenyatta amewataka Wapwani kutofuata mienendo ya kundi la MRC, ambalo hapo awali lilitaka kujitenga na taifa la Kenya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiwahutubia wakaazi wa Kwale siku ya Jumatano, Uhuru alisema kuwa eneo la Pwani kamwe halitajitenga na serikali kuu na kuwataka Wapwani kuondoa fikra hizo.

“Pwani itasalia kuwa Kenya. Msidanganyane kuwa mtajitenga, hizo ni ndoto za mchana,” alisema Uhuru.

Uhuru aidha amewataka Wapwani kupuuza baraza hilo la MRC na kujiandikisha kwa wingi kama wapiga kura ili kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo.

Wakati huo huo, Raisi alisema kwamba serikali ina silaha za kutosha kukabiliana na wahalifu, na kuongeza kuwa juhudi za MRC kutaka kuitenga na Kenya hazitafua dafu.