Raia sita wa Uhabeshi watasalia korokoroni hadi Jumatatu wiki ijayo baada ya kukosekana mkalimani wa lugha ya kiabeshi.
Mekengo Mamush Bekele, Madeo Dejene, Ashore Desalegn, Girma Gabre na Dalalo Chamiso, walipaikana katika eneo la Likoni bila vibali mwafaka vya kuwa humu nchini.
Siku ya Ijumaa, hakimu Diana Mochache, aliagiza kutosomewa mashtaka raia hao hadi pale mkalimani atakapopatikana.
Maafisa wa usalama walipata ripoti kutoka kwa raia na kufaanikiwa kuwatia mbaroni siku ya Alhamisi.