Raia 31 wa Somalia kutoka mjini Mogadishu siku ya Jumanne walifikishwa katika mahakama ya Garissa na kushtakiwa kwa kuwa nchini kinyume cha sheria.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Raia hao, wanaume 23 na wanawake 8, inasemekana walitiwa mbaroni na polisi wa kitengo cha kupambana na ugaidi katika nyumba moja karibu na chuo kikuu cha Garissa, baada ya kupata taarifa kutoka kwa umma.

Kwa mjibu wa afisa mmoja wa ATP eneo hilo, nia ya watu hao hapa nchini bado haijabainika, lakini polisi wanashuku walikuwa wanapanga kuelekea jijini Nairobi.

Hakimu mkaazi Victor Asio amewapiga faini ya shilingi elfu hamsini kila mmoja na kifungo cha miezi sita katika jela.

Wawili wao walikataa mashtaka hayo, na wamewekwa rumande katika kituo cha polisi cha Garissa.

Ni hivi maajuzi tu kaunti ya Garissa iligonga vichwa vya habari, baada ya shambulizi baya sana kutokea katika chuo kikuu cha Garissa, ambapo watu zaidi ya 148, wengi wao wanafuzi, walipoteza maisha yao.

Shambulizi hilo lilitekelezwa na wanamgambo wa Al-Shabaab, na serikali imehapa kuchunguza na kuhakikisha wanamgambo hao wanaadhibiwa.