Raia hao wa Pakistan waliotiwa mbaroni jijini Mombasa siku ya Jumanne. [Picha/ Osman Suleiman]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Raia kumi wenye asili ya Pakstan wametiwa mbaroni jijini Mombasa kwa madai ya kuendesha biashara bila vibali mwafaka.Aidha, raia hao wanakabiliwa na madai ya kuendesha biashara haramu humu nchini.Washukiwa hao walitiwa mbaroni siku ya Jumanne katika maeneo tofauti jijini Mombasa.Akithibitisha kisa hicho, kamanda mkuu wa polisi Kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara alisema raia hao watafikishwa mahakamani ili kufunguliwa mashtaka.“Tutawafikisha mahakamani ili wafunguliwe mashataka,” alisema Ipara.Aidha, Ipara alisema kuwa washukiwa hao wamekuwa humu nchini kwa zaidi ya miaka minne bila vibali.“Hawa jamaa wamekuwa humu nchini kinyume cha sheria kwa zaidi ya miaka minne,” alisema Ipara.Mkuu huyo wa polisi aliitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa sheria kwani wamekuwa wakifanya biashara pasi kutoa ushuru kwa taifa.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6