Raia mmoja wa nchi ya Rwanda ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kuwa nchini bila kibali.
Mahakama iliambiwa siku ya Jumatano kuwa mshtakiwa, Erick Itangihaka, alikamatwa tarehe 18 mwezi Mei katika eneo la feri baada ya kugunduliwa hakuwa na kibali cha kumruhusu kuwa nchini Kenya.
Mshtakiwa huyo alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Teresia Matheka na kuomba mahakama kumsaidia arejee Rwanda.
Hakimu Matheka aliagiza mshukiwa huyo kurejeshwa mahakamani siku ya Ijumaa kupewa hukumu yake.